Advertise here.

unatangazo? weka hapa

Wednesday, 1 January 2014

                  SALAAM ZA MWAKA 2014-01-01
                                    Na: Kapele, H
Kusalimu au kuto kusalimu hakuna maana yoyote kwa watu wanaotaka mabadiliko ya haraka, hasa katika kipindi hiki cha maendeleo ya sayansi na teknolojia. Lakini salamu ni uungwana ndugu zangu nawasalimu kwa salaam za mwaka mpya 2014. Ni matumaini yangu makubwa kuwa kiafya sote tu wazima. Kama ndivyo nasema asanteni.

Ndugu zangu na watanzania wenzangu, nimepata ukakasi sana wa kutaka kulitaja jina langu katika salamu hizi za mwaka 2014. Yote ya yote nilifikiria sana juu ya ng’ombe walio katika nira moja kwa nia ya kukokota jembe ili shamba liweze kuisha, jambo la ajabu ni kwamba ng’ombe hawa hawajuani majina ila mlimi. Najua hunijui nami si kujui ombi langu kwako ni kuwa tuungane ili kulifikisha jembe tulilofungiwa katika fikra zetu ili tufike tupatakapo. Ukiwa msomi au si msomi naomba fungua akili yake twende pamoja katika safari hii ya mwaka 2014, kama u tayari kwenda nami basi ni vema nianze kwa kusema. Dunia uwanja wa fujo, iliwafanya waja wengi kuonekana vichwa maji, na miili yao kuwa ya kutisha mithili ya gamba la nyoka, lililowatia hekaheka na kuwaacha na kichomi cha fikra mbivu na mbichi pamoja na yote hayo 2014 yasema karibu ndani.

E. Kezilahabi (2008), DHIFA katika shairi la WIMBO WA UNYAGO uk. 17, anasema:

Ishi kijana ishi, ishi maisha yako.
Wazee waliishi yao
Sasa yamebaki kwako.
Ukabila ni utumwa
Olewa msichana olewa
Olewa chaguo lako
Hiari ni haki asilia
Achaguaye embe bichi
Ajua lini litaiva.

Basi nami naanzia hapa kuwa mwaka 2014 uwe ni mwaka wa kupanga na kuchagua kwa uhuru juu ya nini wataifa tunataka kifanyike. Kumbuka tu kuwa ni heri kwa kijana aliyechaguliwa ng’ombe wa kulimia ukweni na ng’ombe huyo akalala kuliko kijana aliyechagua ng’ombe mwenyewe katika zizi la ng’ombe wenye afya njema na ng’ombe huyo akalala ni aibu kwake. Ombi langu kwako ni kwamba salamu hizi za mwaka mpya ziwe na wingi wa faraja na hakika kuwa ng’ombe utakaye mchagua hatakutia aibu kama yule aliyekutia mwaka jana. Kijana hasa wewe wa elimu ya juu kaa ukijua kuwa maneno ya mtunzi wa shairi la AKILI alikusudia kukumbusha tu kuwa mwaka huu tuuitao mpya, ni mpya wa namba wala si mambo tuliyoyafanya na tutakayo yafanya ila tu ni mwaka mpya kwa wale wote waliotayari kuifuata kauli hii:

Vinyozi mnyoao chini ya miembe
Andaeni nyembe mpya.
Kuna vichwa vyavingirika
Kutoka maghorofani
Bila ya kujua mtindo wautakao.

Je, msomi au si msomi ni wewe au ni mimi ninaviringika toka ghorofani? Zaidi ya yote mwaka huu ndio jibu la swali hili ni nani hasa anahusika katika unyolewaji chini ya mwembe. Katika hili nachelea kusema kuwa mti ukuliao kivulini si thabiti. Katika salaam hizi ningependa tutumie zaidi mawazo haya nadhani tutafika tupatakapo, shairi la KWA WATU WENYE RANGI, uk. 54 katika Kezilahabi ametajwa anasema:

Simba hafichi mliowe kila wakati awindapo
Hunguruma wanyama wakatawanyika
Kisha akachagua kistahilicho kufukuziwa.

Naye tai huruka juu sana katika uwanja ulio wazi
Na kutua juu ya mti mrefu kuliko yote
Kisha akatazama chini, nchani akiyumba kwa upepo
Halafu hushuka ghafla kuchukua alichokiona kwa makini.

Haki iwapo hatarini
Usifiche uso wako ndani ya umati wenye umoja
Usijifiche blanketini kama kunguni
Ukisubiri usiku kunyonya damu ya jitu lilolala
Kwani likikutupia mkono litakuvunja kwa vidole viwili.

Harufu nzuri ya asali hujumuisha nyuki.
Kipikwacho ndani ya chungu cha umma huliwa adharani.
Watu wote wenye rangi popote mlipo.
Tokezeni hadharani……… kumbukeni kuwa akaaye kimya hupewa kidogo, na asemaye sana hupata kile astahicho. Samba akizungukwa na mbwa mwitu hukimbia. Mwaka 2014 ni mwka wa mabadiliko.

E. kezilahabi anaendelea kutukumbusha tena hasa katika kusherekea mwaka 2014 kuwa: huko nje hakuna tena watu wanaoweza kufikiri. Tunaoweza kufikiri sisi tu tuliomo humu, hasa wakati wa asubuhi. Tufikiri  basi mwaka huu. Kaptula marx uk.13

Pia msanii Mlisho Mpoto katika wimbo wake wa CHOCHEENI, anatukumbusha kuwa mwaka 2014 ni mwaka wa kuchochea kuni mbichi ili moto ukolee, kwani wakati wao wanaendelea kuchambua mavi ya panya katika unga sisi huku tuendelee kuchochea kuni mbichi moto ukolee. Hakusahau kumkumbusha mjomba kuichunguza timu yake kabla ya shindano lijalo. Ni matumaini yangu pia kuwa nawe unayo timu unayopenda ishinde katika shindano hilo. Lakini jambo la muhimu ni kuchagua ng’ombe asiyelala shambani na kama ndivyo heri kulimia mbuzi na shamba likaisha kwa wakati.

Mwaka huu kwako na kwangu uwe ni mwaka wa kuangalia lile wingu ambalo halitembei kuwa ndio alama kuu ya kule tuendako tusije tukapotea, miaka yote baadhi yetu wamekuwa wakipotea njia kwa kukosa dira sasa nakukumbusha tu mwaka huu weka alama ili tufike ng’ambo ile.

Samahani wanangu ni wimbo wa msanii tajwa anatukumbusha wazazi na wale wote tuliowakosea wanaotutegema kuwa sisi ni waleta mabadiliko nasi hatukufanya hivyo basi nenda kwa wote na uwatamkie neno hili samahani. Kwani waneni wanazo semi wazisemazo pasi na soni kuwa bila samahani tuishi bila samahani. Tena wavuvi wa pweza mwambani hukutana. Mimi na wewe tukutane mwambani.

Basi kwa salaam hizi napenda kutoa nafasi kusikia mengi kutoka kwako. Wasalaam 2014, mwaka mpya. Onyo ya mwaka anichezeaye mimi mwaka mpya nitamwacha na ukurutu tena mtupu kifikra na kipesa sasa nakusihi unichangamkie ili yale niliyokuandalia uyapate kama utaki basi wapo watako changamkia fursa hii. Nakutakia mema katika kunitumia. Nakukumbusha tena heri kuandika yale uliyoyapanga maana kusahau kupo ili uweze kufanya mengine.


      



9 comments:

  1. Asante sana ndugu nikuite ndugu kwani sisi Watanzania ni ndugu moja, hongera kwa kutumia maneno yenye hekima na busara lakini mahali pengine umetumia falsafa ngumu,mh ni vyema kwani unafanya tufikiri kifasihi zaidi
    pia nkupe hongera kwa kuingia 2014,mwaka huu ni mwaka wa muhimu kwani safari yetu ya miaka mitatu ndio inatimia tuombeane uzima
    Heri ya mwaka mpya 2014
    MBWAMBO MOSES J
    TEKU/BAED/HK/11744

    ReplyDelete
  2. Kwanza kabisa nikupe hongera kwa kuingia mwaka mpya 2014, asante kwa maneno yako ya busara na ya kifalsafa bwana Kapele jitahidi sana kwani juhudi zako tunazitambua katika kukiendeleza kiswahili,asante kwa maneno ya hekima ,ha ha ha ha kapele kama Mrisho Mpoto,jitahidi zaidi siku moja tuje kusoma kitabu chako
    Heri ya mwaka mpya 2014 wenye mafanikio
    Hamna mafanikio bila juhudi,ugunduzi na sala
    MCHOME HELENA K
    TEKU/BAED/HK/11745.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Asante sana kwa hongera yako nakutakia mafanikio mema katika mwaka huu na Mungu akubariki. asante.

      Delete
  3. Kapele wewe hufai kabisa maana kukusifu nashindwa but you have done I real appreciate it. Keep it up Mr.

    ReplyDelete
    Replies
    1. kaka asante kwa kunitia moya wa kuendelea maneno uliyoyakubali kwani ni kazi kumfanya mtu akubali maneno. asante Mungu akubariki kaka.

      Delete
  4. No communication without channel Kapele keep it use this channel. by kapama@ymail.com

    ReplyDelete
    Replies
    1. I am using this channel brother, thank you very much. wish you all the best.

      Delete
  5. thank you lot for your wish.

    ReplyDelete
  6. MAY GOD BE WITH US SO AS WE CAN COMPLETE OUR STUDIES AND OTHER SOCIAL, POLITICAL AND ECONOMIC ACTIVITIES
    HYERA VITARIA TEKU/BAED/HK/11641

    ReplyDelete

PRONS DJ D69

PRONS DJ D69
THE PRIDE OF TANZANIA

BLOGGERS

BLOGGERS