Advertise here.

unatangazo? weka hapa

Monday 6 January 2014

KAZI YA SINTAKSIA TLK 521

KITIVO CHA SANAA NA SAYANSI YA JAMII

IDARA YA LUGHA NA ISIMU

TLK 521: SINTAKSIA YA KISWAHILI

Kazi ya Pili

Maelekezo

  1. kazi ifanywe na kundi la wanafunzi kumi na tano, na kila mwanafunzi ashiriki kikamilifu.
  2. kazi hii inauzito wa alama 10
  3. kazi ichapwe kwa mwandiko wa Times New Roman, nafasi iwe 1.5
  4. kazi itakusanywa siku ya Ijumaa tarehe 17/01/2014 saa 11:00 – 8:00 mchana.


Swali

Kwa kutumia vyanzo mbalimbali vya maandiko na mitandao, fafanua kwa kina dhana kama vile utawala wa kiuambajengo, kutawala na kutawala kwa karibu, mahusiano ya kutangulia; na mahusiano ya mama, binti na madada.

Na uwanja wa kiswahili



4 comments:

  1. ASANTE KWA UTARATIBU HUU WA KUTUMIA BLOG

    ReplyDelete
  2. UFUPISHO KWA AJILI YA ALAMA 10. Kumbuka swali ni kufafanua, si kueleza wala kuonesha.
    1.Viambajengo ni vijenzi katika sentensi ambavyo hushirikiana na vingine ili kujenga vipashio vikubwa zaidi.
    2.Utawala wa kiuambajengo ni hali ya kifundo cha kijenzi kimoja kukimiliki kifundo kingine.
    3.Kutawala kwa karibu ni hali ya kifundo kikubwa kukimiliki vifundo vingine pasi ukingo kati yake.
    4Mahusiano ya kutangulia ni hali ya neno au kifundo kimoja kujitokeza kabla ya kingine katika ulalo. Yaani kinachokuwa kushoto kinakitangulia kilicho kulia.
    5.Kifundo mama ni kifundo ambacho kinamiliki vifundo vingine. Mfano S ni kifundo mama cha KN na KT.
    6.Kifundo binti ni kile ambacho kinamilikiwa kwa karibu na kifundo mama. Kwa mfano KN na KT ni vifundo binti vya S.
    7Kifundo dada ni kile ambacho kinahusiana na kingine kwa sababu ya kuzaliwa au kumilikiwa na kifundo sawa. Kwa mfano kifundo KN ni dada kwa KT.

    ReplyDelete
  3. Kazi nzuri kwel ted 501 imetuwezesha na tumeweza

    ReplyDelete

PRONS DJ D69

PRONS DJ D69
THE PRIDE OF TANZANIA

BLOGGERS

BLOGGERS